
Isike Samwel
Kwa mujibu wa Isike mwenyewe, filamu hii ndani yake ameshirikisha mastaa mbalimbali akiwepo Hemed Phd na Riyama.
Isike amesema kuwa, mbali na kuonyesha uwezo wake katika kuigiza, filamu hii inabeba mafunzo makubwa kuhusiana na changamoto za kimaisha ambazo zinapelekea mtu wa kawaida kuogopa changamoto za siku zinazofuata.
Isike pia amewataka wapenzi wa filamu kuipokea vizuri filamu aliyoiongoza ya Tulizana, ambayo kwake ni Project kubwa kuwahi kufanya, ikiwa imepangwa kutoka leo hii.