
Taarifa iliyotolewa na mamlaka hiyo leo Disemba 18, imeitaja mikoa ambayo itakuwa na mvua kubwa kuwa ni Njombe, Ruvuma na Morogoro Kusini na kesho Jumatano Desemba 19 maeneo yanayotarajiwa kuwa na mvua ni Rukwa, Mbeya, Songwe, Njombe, Iringa, Ruvuma, Dodoma, Singida, Arusha, Manyara, Kilimanjaro, Tanga, Pwani, Dar es Salaam, Lindi, Mtwara, Morogoro, Unguja na Pemba.
“Kuanzia Jumatatu Desemba 17 hadi Ijumaa Desemba 21 kutakuwa na mvua kubwa ambazo zitasababisha maji kujaa na kupita kwa kasi jambo ambalo ni hatari kwa maisha ya watu", imesema taarifa hiyo.
Taarifa hiyo imeongeza kuwa, “Mamlaka inatoa tahadhari kuwa mvua hiyo itakayoambatana na upepo na kusababisha msongamano wa magari na watu na hivyo kuchelewesha usafirishaji hasa katika maeneo ya mijini, hivyo watu wa maeneo hayo wanapaswa kuchukua tahadhari zitakazoachwa na mvua hiyo mapema".