Jumatano , 20th Mar , 2019

Wakazi wanaoishi mwambao wa ziwa Tanganyika, katika Kijiji cha Itetemya Halmashauri ya mpanda Wilaya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi wanakabiliwa na tatizo kubwa  la kukosa huduma za afya.

Zahanati

Hali hiyo inawalazimu kwenda umbali mrefu  kupata huduma za afya wakati mwingine akinamama wajawazito hujifungulia njiani na wengine kujifungulia majumbani.

Wakazi hao wameiomba serikali kuwatazama kwa ukaribu wananchi hao  kwa kuwafungulia Zahanati  iliyojengwa kwa nguvu zao na msaada kutoka Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF awamu ya tatu, baada ya wananchi hao kuibua mradi huo lakini tangu kukamilka kwake miaka miwili  iliyopita bado haujaanza kufanya kazi kutokana na kutokamilika kwa nyumba ya Mganga Mkuu.

Baadhi ya wakazi hao wakapaza sauti zao kwa serikali kuiomba iweze kuwafungulia zahanati  hiyo ili waweze kupata huduma jirani na kuepusha vifo.

Picha ya Zahanati ya Kijiji cha Itetemya

 

Mwenyekiti wa Kijiji anaizungumziaje Zahanati hiyo

 

Kwa upande wake mwenyekiti wa kijiji cha itetemya ameeleza kwa masikitiko makubwa adha wanazopata wananchi wake, akisema kwamba kwa upande wa TASAF wao walishamaliza kazi yao lakini tatizo linaloikwamisha ufunguzi wake bado haijulikani.