Mkuu wa wilaya ya Dodoma mjini Mh. Patrobas Katambi
Katika mahojiano maalum na EATV & EA Radio Digital ofisini kwake mjini Dodoma, Katambi amesema kuwa wamegundua uwepo wa tatizo hilo hivyo wamekuja na mpango mkakati kwaajili ya kuhakikisha wananchi wanapata huduma.
''Kumekuwa na matumizi ya P2 bila kupata vipimo na ushauri wa daktari hivyo kusababisha madhara ya pengine watu kukosa kuolewa au kukosa watoto, lakini sasa tumekuja na huduma ya Mobile ili watu waweze kupimwa na kupata ushauri kutoka kwa wataalamu popote walipo'', - Amesema Katambi.
Aidha Katambi ameeleza kuwa Wilaya yake kwa ujumla imepiga hatua katika masuala ya huduma za Afya, Elimu na ujenzi wa miundombinu ya kisasa katika kile sekta.
Zaidi tazama Video hapo chini.
