Tessy Chocolate na Lulu Diva
Hii imetokana na kuonekana kwa picha na video zikimuonyesha mrembo na mzazi mwenza wa msanii Aslay aitwaye Tessy Abduly 'Tessy Chocolate' akiwa Dubai aki-enjoy maisha.
Hii ni orodha ya mastaa wa Tanzania waliokwenda Dubai na kurudi Bongo kufanya maajabu katika maisha yao.
Urene Uwoya

Mwezi wa 8 na 9/2018 staa huyo wa kike alionekana akila bata nchini Dubai akiwa na mwanaye wa kiume na msanii Alawi Junior, alivyorudi Bongo maajabu yaliyotokea ni kuachana na aliyekuwa mume wake Dogo Janja pia alifungua ukumbi wake wa starehe jijini Dar es Salaam.
Lulu Diva

Msanii huyu wa kike kuanzia 18/7/2019 alionekana akila bata nchini Dubai hasa kutembelea jangwa maarufu linalopatikana huko, baada ya kurudi Bongo aliandaa tamasha lake siku ya 28 mwezi huo wa saba lilioitwa "The Nighters300".
Ndani ya tamasha hilo alialika mastaa kama Idris Sultan, Haji Manara, Moni Centrozone, Country Boy, Official Nai, Barnaba Classic , Queen Elizabeth Makune Petitman Wakuache na Bonge La Nyau.
Ben Pol
Mkali wa RnB Ben Pize baada ya kuzama katika penzi la Mkenya Anerlisa Muigai, ameonekana akitembea sehemu mbalimbali akila bata ila kuanzia siku ya 28/12/2018 alionekana akiwa Dubai akila raha hadi mwezi wa kwanza 2019.
Alivyorudi mwezi wa 4 alifanikiwa kumvalisha pete ya uchumba mwanamke wake na inasemekana wameshafunga ndoa ya siri, pia ametembelea nchi ya Ufaransa na Marekani.
Tessy Chocolate
Kuanzia siku ya jana alishea picha katika mtandao wa kijamii wa Instagram ikimuonyesha akiwa nchi Dubai akila bata ila watu wanauliza endapo na yeye akirudi atafanya kitu gani.
Mastaa wengine ambao wapo nje ya Bongo wanakula bata na kufanya maisha nje ya Tanzania ni Young Dee (Marekani) Ommy Dimpoz (Dubai) Ray C (Paris,Ufaransa).
