Moni na mpenzi wake Nai
Akizungumza mbele ya kamera za EATV & EA Radio Digital, Official Nai amesema anatamani sana kupata watoto na atafurahi kama itakuwa hivyo.
"Sina mtoto na wala sijawahi kupata mtoto kwenye maisha yangu,hata Mungu akinijaalia nitafurahi sana kwa sababu napenda watoto, nikipata kama watoto 10, 11, 12 itapendeza zaidi yaani nina mpango wa kuzaa sana na kujaza Dunia" amesema Official Nai.
Nai ameongeza kuwa mtoto aliyekuwa naye kwa sasa ni wa Dada yake, ambaye watu wengi wanajua ni wa kwake, lakini ukweli ni kuwa hajawahi kuzaa na Mwanaume mwingine kama inavyosemekana katika mitandao ya kijamii.




