
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhandisi Hamd Masauni
Hayo ameyabainisha leo Februari 5, 2020, Bungeni Dodoma, wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Tauhida Gallos, lililohoji umuhimu wa kufunga CCTV Camera katika vituo vya polisi, zitakazomuwezesha Mkuu wa Kituo kufuatilia na kujua ni nini kinachoendelea kituoni.
"Jeshi la Polisi halina bajeti ya kuwezesha ufungaji wa CCTV Camera vituoni, hivyo Wabunge mshirikiane na wadau ili Camera hizo zinunuliwe zifungwe na kupunguza malalamiko ya huduma isiyo na weledi ya askari kwa wananchi" amesema Mhandisi Masauni.