Jumanne , 4th Aug , 2020

Wahitimu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam wameaswa kutokusubiri kuajiriwa naa Serikali badala yake watumie ufanisi walioupata kujitafutia fursa.

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa William Anangisye.

Hayo yamesemwa leo Agosti 4, 2020, na Makamu Mkuu wa Chuo hicho Prof.William Anangisye wakati akihutubia katika hafla ya Mahafali ya 50 ya chuo hicho.

"Msisubiri kuajiriwa na Serikali bali kuweni wepesi kuangalia ni wapi ujuzi wenu unaweza kutumika kwa ufanisi zaidi, hata kama itabidi ufanye kazi za kujitolea" amesema Profesa Anangisye.

Aidha Profesa Anangisye amewataka wahitimu kuwa watu wakuthubutu na wa kutafuta fursa na si kusubiria fursa ziwafuate kitu ambacho ni ngumu kutokea katika kipindi hiki huku akiwasisitizia kutokukata tamaa na kuwa na ari ya kujaribu hadi wafanikiwe.

Kwa duru ya kwanza ya chuo hicho wahitimu ni 581 huku miongoni mwao 47 wamefuzu shahahada ya uzamivu, 465 shahada za umahiri, 18 stashahada ya uzamili na 51  shahada za awali.