
Mkurugenzi wa hospitali ya Taifa Muhimbili, Prof. Lawrance Mseru
Prof. Mseru ametoa kauli hiyo leo, jijini Dar es salaam, wakati wa mafunzo ya huduma bora kwa watu wanaowahudumia, mafunzo ambayo kwa kuanzia yamewashirikisha walinzi wa hospitali, watoa huduma ya chakula pamoja na watoa huduma ya usafi ndani ya hospitali hiyo.
“Suala la lugha mbaya kwa wateja limekuwa ni changamoto lakini katika kipindi cha miaka miwili iliyopita tumekuwa tukipambana nalo hivyo kupitia mafunzo haya nawasisitiza kulizingatia hilo” amesema Prof Mseru
Aidha amewataka wafanyakazi wa hospitali hiyo kukubali kukaguliwa pale wanapotoka na kuingia hospitalini hapo kwa kuwa huo ni utaratibu uliowekwa na hospitali ili kuzuia hatari na usalama wa wagonjwa na watoa huduma nyingine lakini pia kuepuka uhalifu unaoweza kuzuilika.