Jumatano , 14th Oct , 2020

Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha  Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli amesema jimbo la kawe linahitaji mtu jasiri, mchapakazi, mwenye hofu ya mungu na mwenye kujali maslahi ya Watanzania.

Mgombea urais kupitia CCM Dkt John Pombe Magufuli.

Akizungumza hii leo Oktoba 14, 2020, wakati akihitimisha kampeni zake katika mkoa wa Dar es salaam viwanja vya Tanganyika packers amesema kwa mapendekezo yaliyotolewa na viongozi wa CCM, Joseph Gwajima anafaa kuwa mbunge wa Kawe.

''Ninataka kawe ibadilike,nataka kawe tutengeneze ajira za vijana,kwanini Kawe hakuna viwanda vingi wakati Pwani kuna viwanda vya kutosha mpaka Mkuranga vimejengwa'', amesema Dkt. John Magufuli

Pia Dkt Magufuli ameongelea haya, ''Tumepanga kujenga viwanda vya kuchakata samaki, kwanini visijengwe Kawe, vijana wetu wakapata ajira? tunahitaji mtu mwenye mipango, tunahitaji mtu mwenye 'connection' na serikali''. 

Joseph Gwajima ni mgombea wa Kawe kupitia CCM akichuana kwa ukaribu na mgombea wa CHADEMA Halima Mdee, kupitia jimbo hilo