
Mratibu wa klabu ya Simba, Abbas Ally(Kulia) akimkabidhi jezi Abbas Tarimba(kushoto) ambaye ni mkurugenzi wa utawala wa Sportpesa ambao ni wadhamini wa mabingwa hao wa VPL.
Katika mchezo ambao Simba ilifungwa bao moja kwa sifuri, utata uliibuka kwa baadhi ya wafuatiliaji wa mchezo wa mpira wa miguu baada ya kuona Jonas Mkude akivaa kitambaa cha unahodha badala ya Mohamed Hussein ambaye katika kikosi cha wachezaji kilichotajwa ndiye aliyeorodhoshwa kuwaongoza wenzake.
Mratibu wa Simba, Abbas Ally amesema hakuna sheria katika soka inayolazimisha kuwa mchezaji aliyechaguliwa kuiongoza timu hawezi kubalishwa.
''Nahodha wa Simba ataendelea kuwa John Bocco na msaidizi wake ni Mohamed Hussein Tshabalala, lakini katika mpira wa miguu sio lazima hao tuliowachagua ndio wavae kitambaa cha unahodha,.
Katika mchezo dhidi ya Ruvu Shooting wachezaji waliamua kumteua Jonas Mkude kwakuwa waliona pengine Tshabalala si muongezaji sana na ikizingatiwa mechi ilikua na presha kubwa''. alisema Abbas Ally.
Vilevile, Abbas amesema wamekaa kwa pamoja na kutathmini mwenendo wao katika ligi na ni imani yao timu itaanza kupata matokeo mazuri kwa mechi zijazo.