Jumatatu , 21st Dec , 2020

Jaji mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahimu Juma amewataka mawakili 166 wapya walioapishwa leo kuziishi kanuni na maadili akiwataka kuwajibika kwa mujibu wa Katiba ya nchi ambayo ndiyo sheria mama akiwataka kutojihusisha na vitendo vya ujanja ujanja.

Jaji mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahimu Juma

Jaji Mkuu ametoa rai hiyo katika hafla ya kuwapokea mawakili wapya 166 ambapo amewataka  kusimamia misingi ya haki ili kuisaidia mahakama kufikia maamuzi ya kesi mbalimbali za wateja wao kwa wakati.

''Kwa sasa changamoto ya ajira ni kubwa katika dunia ya ushindani duniani unakuwa kwa kasi teknojia ukichukua nafasi hivyo mawakili hawana budi kupambana na changamoto hii''. Prof Ibrahimu Juma

Aidha amewaonya Mawakili ambao wamekuwa wakifanya vitendo vya uchochezi katika mitandao ya kijamii kwa kutumia majina halisi na wengine majina yasiyo halisi  ambao wamekuwa wakikosoa kanuni na sheria zilizowekwa