
Wa pili kulia Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi akiwa kwenye Ziara yake mkoani Mbeya
Naibu Waziri amechukua uamuzi huo kufuatia kutoridhishwa na utendaji kazi wao baada ya kukuta changamoto nyingi katika wilaya ya Mbarali huku wakishindwa kuchukua hatua sahihi kuzitatua, ikiwemo kutoa taarifa zisizo sahihi kuhusiana na utekelezaji na uendeshaji miradi ya maji.
Mhandisi Mahundi amesema wananchi wa wilaya ya Mbarali wana kero nyingi kuhusiana na huduma ya maji huku wasimamizi wakishindwa kuwahudumia badala yake wakitoa taarifa zilizo tofauti ukilinganisha na uhalisia wa hali iliyopo, jambo linalokwamisha jitihada za serikali kutatua kero za wananchi.
Aidha Naibu Waziri huyo ametangaza kuivunja Bodi ya ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira ya Mji Mdogo wa Rujewa katika wilaya ya Mbarali, mkoani Mbeya kwa kushindwa kuisimamia ipasavyo menejimenti ya mamlaka hiyo kutimiza majukumu yake kwa ufanisi kutokana na kubaini ukosefu wa huduma ya uhakika ya maji kwa muda mrefu kwa wakazi wa mji huo bila sababu za msingi.