
Picha kubwa ni baba mzazi wa msanii Young Killer, Mzee Msodoki
Mzee Msodoki amesema mama Young Killer aliamua kumwambia hivyo mtoto wao kwa sababu aliumizwa na kitendo cha Mzee Msodoki kuukimbia ujauzito wa msanii huyo kabla hajazaliwa na kwenda kuishi nchini Congo DR.
"Mama Young Killer nilikuwa nakaa naye jirani kule Mwanza, wakati huo nilikuwa nafanya kazi Saloon, tukawa kwenye mahusiano ambayo yalidumu kama miezi 6 na baadaye akaniambia ana ujauzito, sasa kwa wakati huo mimi nilikuwa sijajiandaa kulea na majukumu hivyo nikapata safari ya kwenda Congo nilivyorudi sikumkuta" ameeleza Mzee Msodoki
"Nimekuja kugundua kama mtoto yupo na ameshakuwa mkubwa ila mama yake alishamwambia kwamba baba yake ameshakufa wakati mimi nipo, ndiyo maana hata yeye haamini kama mimi ndiyo baba yake kweli" ameongeza
Mzee Msodoki amesema aliwahi kukutana na Young Killer na alimwambia kama yeye ndiyo baba yake lakini alijibiwa kwamba hana shida lakini mpaka mama yake amdhibitishie.