
Nyota wa Juventus, Cristiano Ronaldo.
Akizungumza na kituo cha habari cha DAZN cha nchini Marekani mchana wa leo tarehe 25 Machi 2021, Nedved amejibia sakata la Ronaldo kuhusishwa kuihama klabu hiyo na kurejea Real Madrid ya Hispania kwa kusema:
“Ronaldo ana mkataba hadi tarehe 30 Juni 2022 na atabakia.”
“Kitakachotokea siku za usoni kila mtu atakiona. Cristiano anatupatia nafasi kubwa ya kwenda mbele kote, kiufundi na kimasoko. Kwa upande wa kiufundi, hakuna chakuthibitisha zaidi kwani tayari ameshafunga mabao 100 kwenye michezo 120”.
Maneno hayo ya Makamu wa Rais wa Juventus yanamaliza uvumi kwa sasa unaoenea kuwa nyota huyo yu mbioni kurejea klabu yake ya zamani ya Real Madrid ya Hispania aliyoikacha miaka miwili iliyopita na kutua Juventus.
Ronaldo tokea atue Juventus, ameshafunga mabao 95 na kutengeneza mengine 22 kwenye michezo 123 ya michuano yote, hivyo amehusika kwenye mabao 117 kwenye michezo 123 aliyoichezea Juventus kwenye michuano rasmi.
Kwa msimu huu pekee, CR7 ameshafunga mabao 30 na kutengeneza mabao 4 katika michezo 34 katika michuano yote, ni sawa na kusema, Ronaldo amehusika kwenye mabao 34 katika michezo 34 ya michuano yote akiwa na Juventus kwa msimu huu pekee.