Jumapili , 28th Mar , 2021

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amemsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA), Eng. Deusdedit Kakoko kuanzia leo Machi 28, 2021.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan

Rais ametangaza maamuzi hayo leo Machi 28, 2021 wakati wa hotuba yake baada ya kupokea ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) za mwaka wa fedha 2019/2020 na kubaini kuwepo kwa ubadhirifu mkubwa katika mamlaka hiyo.

''Kuhusu bandari kumekuwa na mwendelezo wa ubadhirifu na nafahamu Waziri Mkuu alitembelea pale na kuunda kamati ya uchunguzi lakini waliofukuzwa ni watendaji wa chini, sasa natoa agizo la kumsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari kuanzia leo,'' amesema Rais Samia.

Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Eng. Deusdedit Kakoko

Mbali na kumsimamisha Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Eng. Deusdedit Kakoko, amemwagiza CAG Charles Kichere pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU kuendelea kufuatilia kwa ukaribu juu ya mwenendo wa utendaji kazi na uwajibikaji ndani ya Bandari.

Zaidi tazama video hapo chini