Jumatano , 14th Apr , 2021

Matajiri wa jiji wa Manchester, Klabu ya Manchester City saa 4:00 usiku wa leo Aprili 14, 2021 itacheza ugenini kwenye uwanja wa Signal Iduna nchini Ujerumani kucheza dhidi ya Borrusia Dortmund kwenye mchezo wa mkondo wa pili wa michuano ya klabu bingwa Ulaya.

Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola.

Manchester City wanafaidia ya kuongoza mabao 2-1 kwenye mchezo wake wa kwanza aliocheza kwenye dimba lake la Etihad kwenye mchezo ulionesha upinzani wa hali ya juu na kulazimika City kupata ubao la ushindi dakika za lala slama.

Kuelekea kwenye mchezo huo, kocha wa Manchester City, Pep Guardiola amepania kutinga hatu aya nusu fainali kwa mara ya kwanza na timu yake hiyo na kuwasisitiza wachezaji wake kufanya hivyo kwani ameambulia 16 bora mara moja na kuishia robo fainali mara tatu.

“Sasa ni muda wa kupiga hatua inayofuata. Kila mmoja anataka hivyo. Wachezaji wanataka kufanya hivyo kwasababu walijisikia vibaya sana waliposhindwa kucheza nusu fainali na hii ndiyo nafasi ya kulithibitisha hilo miongoni mwao”.

“Lakini hayupo mtu wakutupatia hiuyo nafasi, tunapaswa tuishinde, tunatakiwa tufanye hivyo. Tukiwa kwenye hatua hii ya robo fainali hayupo atakayetusemea mazuri tofauti na tukifika nusu fainali. Kama ni wazuri tutaenda kufanya hivyo”. Akasisitiza hivyo, Pep.

Kwa upande wa Borrusia Dortmund, kocha wa timu hiyo Edin Terzic amemkingia kifua mshambuliaji wake kinda, Erling Braut Haaland kuwa ni muhimu kikosini hapo lich aya kwamba hajafunga kwenye michezo yake sita ya mwisho.

Lakini kuzungumzia mchezo huo kiujumla, Terzic amesema “Ilituumiza sana  kuruhusu bao dakika za mwisho na tunahitaji ushindi, tunajua hilo na haitoshi pekee kujilinda zaidi. Tunapaswa kutengeneza nafasi na kuwa hatari zaidi”.

“Utaenda kuwa mchezo mgumu lakini tunajiamini, japo kuwa imani hii peke haitoshi”.

Kuhusu hali ya vikosi, Dortmund wanataraji kucheza bila Jadon Sancho mwenye majeraha huku Matts Hummels na Marco Reus wakiwa mashakani kucheza mchezo huo. City wamaemjumuisha kikosini, Aymeric Laporte baada ya kupona majeraha yake wakati Sergio Aguero akikosekana.