Jumatano , 11th Aug , 2021

Member wa kundi la Wagosi wa Kaya kutoka Tanga Mkoloni amesema hawajaacha mziki na hawawezi kuacha kwa sababu mziki ndio umefanya kuwaunganisha na jamii licha ya kukaa kimya kwa muda mrefu sasa.

Picha ya Wagosi wa kaya kulia ni Dkt John kushoto ni Mkoloni

Mkoloni amesema endapo Wagosi wa kaya wakiacha muziki itakuwa wamekataa muunganiko wao na jamii kitu ambacho hakiwezekani hivyo wataendelea kufanya mziki.

"Ni muda mrefu tumekaa nje ya game lakini Wagosi wa Kaya hatuwezi kuacha muziki kwa sababu umetuunganisha na jamii  ina maana tukiacha itakuwa tunakataa muunganiko wetu na jamii kitu ambacho hakiwezekani" amesema Mkoloni

Wakali hao wameshatoa ngoma kali zilizofanya vizuri kama wauguzi, traffic huyo, gahawa, walimu tuna hali ngumu na bao.