Jumatatu , 23rd Aug , 2021

Mchezo wa ligi kuu ya Ufaransa 'Ligue 1' kati ya Lille na Olympic Merseille umehairishwa baada ya baadhi ya mashabiki wa klabu ya Nice kuvamia eneo la kuchezea 'pitch' na kupelekea fujo zaidi na wachezaji wa Merseille jambo lililopelekea mwamuzi Benoit Bastien kuhairisha mchezo huo.

Baadhi ya mashabiki wa klabu ya Nice ya Ufaransa wakionekana wakivamia uwanja na kufanya vurugu dhidi ya wachezaji wa klabu ya Merseille kwa kuanza na Dimtri Payet.

Kisa cha fujo hizo ni baadhi ya mashabiki wa Nice walioamua kumpiga na chupa ya maji mchezaji wa Merseille, Dimtri Payet dakika ya 74 na mchezaji huyo kupata maumivu hadi kudondoka chini na hatimaye Payet akaamua kujibu mapigo kwa kuikota na kuwarushia mashabiki hao ambao waliruka uzio kumvamia mchezaji huyo na wachezaji wengine wa Maerseille.

Hatma ya mchezo huo uliochezwa Jumapili ya jana Agosti 23, 2021 kwenye dimba la Allianz Riviera uwanja wa nyumbani wa klabu ya Nice bado haijajulikana kama utamaliziwa kwa dakika 16 zilizosalia ama laa.

Nice ipo nafasi ya 6 ikiwa imecheza michezo 2 na kupata alama 4 baada kufungwa mchezo mmoja na kutoka sare mchezo mmoja ilhali Merseille wapo nafasi ya nane wakiwa wamecheza michezo 2 na kupata alama 4 kama Nice.