Jumanne , 31st Aug , 2021

Buti alilovaa Burna Boy kwenye show yake siku ya Ijumaa huko uingereza katika ukumbi wa O2 Arena, limezua gumzo mitandaoni kutokana na muonekano wake wa kipekee.

Picha ya Masanii Burna Boy

African Giant alivalia buti rangi nyeusi kutoka kampuni ya mavazi ya Rick Owens ya Marekani ambayo inajihusisha na ubunifu, uzalishaji, usambazaji na uuzaji wa mavazi yao ambayo yamekuwa maarufu kutokana na upekee wake.

Mavazi hayo kwa kiasi kikubwa hutumiwa na watu maarufu kama models, wanamuziki na waigizaji kutokana na gharama kuwa juu na ndio maana ni nadra sana kuona watu wa hali ya chini wakitumia bidhaa zao.