Jumatano , 1st Sep , 2021

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Nchemba amesema tangu kuanza kwa tozo mpya za miamala takribani muda wa mwezi mmoja na nusu jumla ya Shilingi Bilioni 63 zimekusanywa na zimesaidia miradi mbalimbali ikiwemo Vituo vya Afya 70.

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Nchemba

''Tangu tozo mpya zimeanza tumekusanya zaidi ya Shilingi Bilioni 63 kwa muda tu wa mwezi mmoja na nusu,'' amesema Dk. Nchemba.

Aidha ameongeza kuwa, ''Kwa mwezi mmoja na nusu wa makusanyo ya tozo mpya, tumejenga vituo vya afya katika tarafa 70 ambazo hazikuwa navyo kwenye tarafa 217 tangu kupata uhuru na hivi vina jengo la upasuaji, maabara. Mh. Rais anakwenda kuokoa maisha ya wajazito wengi sana,” amesema Dk. Nchemba.

Kwa upande mwingine  ameeleza pia kuwa, ''Kabla ya kuanza hizi tozo mpya za miamala nchini kwa mwezi ilikuwa  Mil. 10 hadi 11. Tulipoanza imekuwa Milioni 10 hadi 9.1, unaweza kuona ni kama ilivyokuwa kabla hatujaanza utekelezaji na imekuwa hivi hadi tarehe za mwisho kabisa yaani Agosti 29'.

Tazama Video hapo chini