Jumapili , 12th Dec , 2021

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro ametangaza rasmi kuwa wafugaji watakaothubutu kuingiza mifugo katika Hifadhi ya Jamii ya Wanyamapori ya ILUMA watatozwa faini ya Sh. 100,000 kwa kila kichwa cha ng'ombe baadala ya Sh. 50,000 iliyokuwa ikitozwa mwanzo.

Kundi la ng'ombe

Hatua hiyo inachukuliwa ili kuondoa malalamiko ya wafugaji kutozwa tozo mbili tofauti pindi mifugo inapokamatwa imeingia katika hifadhi hiyo.

Akizungumza na na Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama pamoja na wajumbe wa Kamati ya Siasa ya wilaya ya Ulanga, mkoani Morogoro,  Dkt. Ndumbaro amesema amefikia uamuzi  huo ili kuwapa nafasi wafugaji wataokamatwa wakiwa wameingiza mifugo yao kati ya Hifadhi hizo  kuamua kulipa kiasi hicho cha pesa kwa Uongozi wa Hifadhi ya Taifa ya Nyerere au  kwa Uongozi wa Hifadhi ya Jamii ya Wanyamapori ya ILUMA kwa vile kote faini ni sawa.

'' Kwa mamlaka niliyonayo kama Waziri mwenye dhamana natangaza kuanzia leo faini ni kiasi cha shilingi laki moja kwa kila kichwa cha ng'ombe'', amesema Dkt. Ndumbaro.