Alhamisi , 16th Dec , 2021

FC Barcelona inaripotiwa inamuwinda mshambuliaji wa Manchester City Ferran Torres kama mbadala wa Sergio Kun Aguero aliyestaafu kucheza soka akiwa na umri wa miaka 33 kutokana na matatizo ya Moyo, baada ya kushauriwa na Madaktari.

Ferran Torres

Kwa mujibu wa ripoti kutoka nchini Hispania zinadai kuwa kwa sasa Torres hana furaha ndani ya Manchester City kutokana na kutopata nafasi ya kucheza mara kwa mara hivyo Barcelona wanaamini wanaweza kumpata endapo kama watamuahakikishia nafasi ya kucheza.

Mshambuliaji huyo raia wa Hisapnia mwenye umri wa miaka 21, alijiunga na Manchester City msimu uliopita wa 2020-21 akitokea Valencia na alicheza michezo 36 na kufunga mabao 13 kwenye mashindano yote lakini msimu huu mpaka sasa amecheza michezo 7 kwenye mashindano yote na kafunga mabao 3 tu.

Baada ya kustaafu kwa Aguero Barcelona wamesaliana na washambuliaji wa kati wawili wenye uzoefu ukiachana na vijana ambao ni Luuk de Jong na Martin Braithwaite, Braithwaite kwa sasa anamajeruhi wakati De Jong hayupo kwenye kiwango kizuri kwa sasa, kna kocha Xavi amejikuta akiwatazama zaidi vijana kama Yusuph Demir, Ansu Fati na washambuliaji wa pembeni Ousmane Dembele na Memphis Depay.