Kaburi la mtoto Christian Samson lililofukuliwa
Simanzi na huzuni zilitawala katika makaburi hayo hii ikiwa sio mara ya kwanza vitendo hivyo vya ufukuaji wa makaburi kujitokeza, na mara hii imejitokeza hali isiyokuwa ya kawaida kwa kuwa mwili marehemu umetafutwa kwa zaidi ya saa manne huku jitihada hizo zikishindikana.
Kufuatia hali hiyo imemlazimu Mkuu wa wilaya ya Rahabu Mwagisa, na kuzungumzia vitendo hivyo huku akisisitiza suala la maombi kuwa ni la muhimu na jeshi la polisi linafuatilia ili kuwabaini waliohusika na kitendo hicho.