Jumamosi , 29th Jan , 2022

Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Arusha SP Solomon Mwangamilo, amewataka madereva wa magari ya serikali kufuata sheria za barabarani ili kupunguza ajali na kuvichukulia vyombo hivyo kama vyao na kuacha tabia ya visingizio kwamba hulazimishwa na wakubwa wao kuendesha hivyo.

Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Arusha SP Solomon Mwangamilo

SP Mwangamilo, amewataka pia madereva hao kuacha visingizio hivyo, badala yake wawe washauri wazuri kwa mabosi zao kwa kuwaambia ukweli kwamba endapo wakiendesha kwa kasi kubwa wanaweza kusababisha ajali.

"Wewe ni mshauri wa kiongozi, mshauri kwa hekima kwamba barabara hii sio rafiki kama tukienda kwa kasi tunaweza kupata ajali, overspeeding ni jambo ambalo unaweza kuli-manage, nasema tuache visingizo kwamba nililazimishwa," amesema SP Mwangamilo