
Mbunge wa jimbo la Mbogwe Nicodemas Maganga
Kauli hiyo ameitoa hii leo Mei 11, 2022, bungeni jijini Dodoma na kuongeza kuwa waangalie mifano kutoka mataifa mengine yanayotumia lugha zao hadi kwenye vyombo vya habari.
"Mimi ni Msukuma lugha yangu mkiipa nafasi mkaweka kwenye system, Kisukuma kikiingia kwenye computer Wachina watakuja kujifunza hapa, hata Wazungu wakija kwenye migodi yetu wakakuta Askari wanazungumza Kisukuma tu hiyo hali itawafanya wakisomee, lazima tukae tufikirie tunawachenga vipi kwenye huu ulimwengu wa kutafuta pesa," amesema Mbunge Maganga