
Dkt. Chana ameyasema hayo Jijini Arusha aliposhiriki ibada katika kanisa la KKKT Dayosisi ya Kaskazini Kati, Usharika wa Arusha Mjini.
Amesema mkoa wa Arusha umebarikiwa na Mungu kwa kuwa na vivutio vingi vya Utalii hivyo wananchi wanatakiwa wazilinde baraka hizo za vivutio kwa kuvitunza.
Akitoa salamu kwa niaba ya waumini wa kanisa hilo Mchungaji Kiongozi Rachel Axwe amemwomba Waziri Chana kumfikishia salamu Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa na nzuri anayoifanya ya kuitangaza Tanzania kupitia Sekta ya Utalii na kuhamasisha uwekezaji hali inayowanemeesha pia wakazi wa jiji la Arusha ambao kwa asilimia kubwa wanategemea Biashara ya Utalii.
Waziri Chana yupo jijini Arusha kwa ziara ya Kikazi.