Jumanne , 30th Aug , 2022

Wizara ya Afya imesema ipo mbioni kukamilisha mpango wa manunuzi ya dawa moja kwa moja kutoka viwandani ikiwa ni katika jitihada za kupunguza makali ya gharama za vifaa tiba na dawa ambavyo vimekuwa vikipelekea gharama kubwa za matibabu kwa wananchi.

Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel

Akizungumza hii leo Agosti 30, 2022, wakati akifungua ķongamano la vifaa tiba na dawa kwa nchi za Afrika Mashariki, Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel, amesema serikali kwa sasa itakuwa ikinunua dawa moja kwa moja kutoka kwa wazalishaji baada ya watu wa kati kuwa na mtindo wa kupandisha bei za vifaa tiba na dawa hali inayoongeza gharama kubwa na mzigo kwa wananchi.