Wakili Mkuu wa Serikali Dkt Boniphace Luhende
Akizungumza jijini Dar es Salaam ikiwa ni siku yake ya kwanza tangu kuapishwa baada ya kuteuliwa na Rais kuwa Wakili Mkuu wa Serikali Dkt.Luhende amesema kwa kufanya hivyo kutasaidia kumaliza migogoro kwa wakati kwa kufuata haki na sheria kudumisha uhusiano kati ya serikali na wawekezaji kujenga imani kwa wawekezaji kuhusu hali ya utoaji haki nchini
Kwa upande wake Naibu Wakili Mkuu wa serikali Sara Mwaipopo, amesisitiza kuzingatia kwa kanuni sheria na taratibu kwenye eneo la matumizi ya fedha za serikali na kwenye maeneo yote ambayo wanatakiwa kuyasimamia.
Akitoa taarifa za utendaji kazi ndani ya ofisi hiyo Mkurugenzi wa Utawala James Kibamba, amesema idara zilizopo ndani ya ofisi hiyo zimekuwa zikionesha jitihada kubwa kwenye utekelezwaji wa majukumu yake licha ya kupanbana na changamoto nyingi ambazo nyingine zipo nje ya uwezo wao.