Jumanne , 1st Nov , 2022

Hatimaye familia ya kijana Ibrahim Shakiru aliyeuawa kwa kupigwa na walinzi pamoja na wananchi wenye hasira kali Kirumba jijini Mwanza, wameamua kuuzika mwili wa kijana huyo huku Imamu wa msikiti wa Muumin Kabuhoro akiwataka kumuachia Mungu aweze kuhumu.

Mazishi ya kijana Ibrahim Shakiru

Wakati mwili wa kijana Ibrahim Shakiru aliyekuwa na umri wa miaka 16 ukipumzishwa katika nyumba yake ya milele Sheikh Rashidy Juma wa msikiti wa Kabuhoro Kirumba akawasihi waumini wengine kuendelea kumcha mwenyezi Mungu na kujiandaa vyema na safari hiyo huku Imamu wa msikiti wa Kabuhoro Rashidy Juma akisema wanamuachia Mungu aweze kuwahukumu waliohusika na tukio hilo

‘hakuna mtu ambae atakaa hapa duniani milele bali tunakaa kwa muda na muda ukifika kama si mimi basi ni wewe  tutaondoka katika Maisha haya tuendelee kuomba na kumuombea kijana wetu maana hii ni safari ina-kuja kwa ghafla’ – amesema Rashidy Juma Imamu msikiti wa muumin Kabuhoro Kirumba

Tausi Jackson ambaye ni rafiki yake na Ibrahimu amesema marehemu Ibrahim Shakiru alikuwa ni kajana mtulivu na mpole huku Jirani yake Gervas Manase akitoa ushauri kwa vijana wengine kuacha kutembea hovyo na silaha.