Alhamisi , 3rd Nov , 2022

Serikali imesema kwamba inaendelea na uchunguzi ili kubaini chanzo hasa cha moto Mlima Kilimanjaro, ambao kwa sasa umedhibitiwa kwa kiasi kikubwa ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa

Kauli hiyo imetolewa leo Novemba 3, 2022, Bungeni jijini Dodoma na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, wakati akitoa kauli ya serikali kuhusu moto huo.

"Serikali inaendelea kuchunguza chanzo cha moto katika Mlima Kilimanjaro, ili kuchukua hatua stahiki, jitihada za udhibiti wa moto zimefanyika kwa ushirikiano na wadau mbalimbali hadi leo Novemba 3 zoezi la uzimaji wa moto linaendeklea vyema na moto kwa kiasi kikubwa umedhibitiwa katika maeneo korofi," amesema Waziri Mkuu