Jumatatu , 19th Dec , 2022

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango, amewaagiza viongozi wa mabonde ya maji nchini kuwachukulia hatua wale wote walioziba mto Ruaha bila vibali sahihi vya matumizi ya maji ikiwa ni pamoja na kubomoa walipoziba kwa gharama zao.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango

Maagizo hayo ameyatoa hii leo Desemba 19, 2022, mkoani Iringa, wakati wa kongamano la mazingira lililowakutaniasha wahariri wa vyombo vya habari, waandishi wa habari pamoja na wadau mbalimbali wa mazingira nchini katika hatua ya kuboresha mazingira hususani vyanzo vya maji ikiwemo mto Ruaha Mkuu.

"Chukueni hatua leo, wale walioziba mto Ruaha bila vibali sahihi bomoeni kwa gharama zao, nyie viongozi wa mamlaka za maji kwa wale ambao wamejenga hivyo vizuizi vya maji na mliwapa vibali nataka kuviona mniletee," amesema Makamu wa Rais