Jumapili , 5th Feb , 2023

Wanafunzi wa shule ya sekondari Igelegele na Mahina wameishukuru serikali kuwaondolea adha ya msongamano madarasani kwa kuwaongezea vyumba vya madarasa na walimu hali inayopelekea kusoma katika mazingira mazuri huku wakiahidi kufanya vizuri katika mitihani yao

vyumba vipya vya madarasa vilivyojengwa katika Shule ya sekondari Igelegele Mwanza.

Shule ya sekondari Igelegele hapo awali ilikuwa na vyumba vya madarasa vinne ikiwa na wanafunzi 110 kwa sasa kuna wanafunzi 1201 vyumba vya madarasa vikiwa 29 na walimu 22, huku katika shule ya sekondari Mahina waKianza na vyumba vitano na hadi sasa vimeongezeka kufika vyumba 18.

Awali akikagua vyumba hivyo vya madarasa mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM mkoa wa Mwanza Sixbet Reuben amesema Rais Samia amedhamiria kuwapa mazingira mazuri ya kujifunzia wanafunzi wote nchini wakiwemo na wanafunzi wa mkoa huo wa Mwanza