Jumatatu , 6th Feb , 2023

Jeshi la Kujenga Taifa JKT limesema vijana 147 waliokutwa na maambukizi ya VVU si wale ambao tayari wapo ndani ya mafunzo ya jeshi hilo kama wengi wanavyodhania na kukemea baadhi ya vyombo vya habari kutumia picha za vijana ambao si wahusika na kuzua taharuki kwa jamii.

Mkuu wa Tawi la Utawala JKT Brigedia Jenerali Hassan Mabena

Taarifa hiyo imetolewa na jijini Dodoma na Mkuu wa Tawi la Utawala JKT Brigedia Jenerali Hassan Mabena, na kusema Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Masuala ya Ukimwi kwa kipindi cha Februari 2022 hadi Februari 2022 iliyowasilishwa wiki iliyopita.

Katika hatua nyingine Brigedia Jenerali Hassan Mabena amesema wale waliokutwa na maambukizi ya VVU walipatiwa huduma za kiafya ikiwa ni pamoja na kupewa ushauri nasaha na wengine wakaanzishiwa dawa za kufubaza ugonjwa huo.

Ikumbukwe kuwa wiki iliyopita Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Masuala ya Ukimwi ililitaarifu Bunge kuwa vijana 147 kati ya 67,299 waliojiunga na Jeshi la Kujenga Taifa JKT kwa mujibu wa sheria katika kipindi cha miaka mitatu wamekutwa na maambukizi ya Virusi vya  Ukimwi (VVU) sawa na asilimia 0.22 kwa vijana waliomaliza kidato cha sita nchini na kuitwa kujiunga na JKT katika kipindi cha 2019, 2020 na 2021.