Leo wazazi wa watoto hao wamefika kwenye ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mwanza na kufanikiwa kuzungumza na katibu tawala wa mkoa huo Elikana Balandya ambae amewaambia kwa taarifa waliyopewa kutoka baraza la mitihani inasema shule ya sekondari Thaqaafa haikufanya udanganyifu wa mitihani ya kidato cha nne bali wanafunzi ndiyo walifanya udanganyifu na kufutiwa matokeo
"Watoto 333 nchi nzima wamefuti wa matokeo wakiwemo na hawa vijana wetu 140 wa thaqaafa katika maelezo ambayo serikali ya mkoa imeyapata ambayo yamepelekwa kwa mkuu wa shule katika taarifa hiyo imethibitika hawa Watoto 140 wamefanya udanganyifu kwenye masomo ya historia, civics na biologia"
Katika hatua nyingine katibu tawala huyo amesema watumishi watano wa serikali waliohusika kwenye udanganyifu huo awamesimamishwa kazi
"Serikali imeshawasimamisha kazi watumishi wake watano ambao walibainika kuhusika na udanganyifu huo wa mitihani kwahiyo ni muhimu kwetu sisi wazazi tukatambua hilo kwamba ni udanganyifu ulifanyika kwenye hayo masomo"
Baada ya ufafanuzi huo kutoka kwa katibu tawala mmoja wa wazazi wa Watoto hao wakatoa ya moyoni
"Lazima tuungane tufungue kesi ya jinai mahakamani sababu shahidi wa kwanza ni wafanyakazi wake waliothibitika kwenye wizi huo kwahiyo tutashtaki wafanyakazi wake na washtakiwa wa pili watakuwa ni shule husika hiyo tutasimama mahakamani na mawakili watakuwepo na dhamira yetu kufika baraza la Taifa tupate maelezo kwa Adolf Mkenda"
