Kimbunga Gabrielle kinatarajiwa kukipiga kisiwa cha Kaskazini mwa nchi hiyo kuanzia leo usiku m na kinaweza kuleta upepo mkali na mvua kubwa zaidi.
Wakazi wametakiwa kuhakikisha wanapata mahitaji ya kutosha kudumu kwa siku tatu iwapo watakwama nyumbani.
Kimbunga hicho kinajiri wiki kadhaa baada ya mvua kubwa kunyesha katika mji wa Auckland.
Makazi ya kuwahamisha watu yameanzishwa huku shirika la ndege la taifa, limefuta safari kadhaa za ndani kabla ya kuwasili kwa kimbunga hicho.

