Alhamisi , 23rd Feb , 2023

Siku ya mwisho ya kampeni inaendelea nchini Nigeria kabla ya uchaguzi wa urais wa Jumamosi wiki hii. Wagombea watatu wanadaiwa kuwa na mabadiliko ya ushindi katika taifa hilo lenye idadi kubwa ya watu barani Afrika.

 UchaInasemekana kuwa huu ni uchaguzi wenye ushindani mkubwa zaidi tangu kumalizika kwa utawala wa kijeshi mwaka 1999. Pande zote zimeahidi kutatua migogoro yoyote kupitia mahakama.

Mbali na wagombea kutoka vyama vikuu viwili , chama tawala cha All Progressives Congress na Peoples Democratic Party , mgombea wa tatu anayeongoza ameibuka.

Bw.Peter Obi wa chama cha Labour ameonekana kuwa na mvuto na kupata  uungwaji mkono mkubwa kutoka kwa wanaharakati vijana kwenye mitandao ya kijamii.

Wakati hayo yakijiri Mgombea wa seneta wa Nigeria aliuawa siku ya jana kwa kupigwa risasi na mwili wake kuchomwa moto na washambuliaji wakati akiwa njiani kutoka kwenye mkutano wa kampeni katika jimbo la kusini la Enugu

Wasaidizi wake waliokuwa naye pia waliuawa kwa kupigwa risasi kabla ya gari lao kuchomwa moto huku miili ikiwa ndani, vyombo vya habari nchini humo vimeripoti