
Amesema hiyo imetokana na ufatiliaji duni na kutofanyika kwa usuluisho wa hesabu mara kwa mara.
Kichere pia amesema licha ya Wakusanyaji mapato katika Mamlaka 98 kutowasilisha Bilioni 11.07, Mawakala wa Mapato katika Mamlaka nyingine 10 za Serikali za Mitaa pia hawakuwasilisha Benki kiasi cha Shilingi Bilioni 4.12.
Kufuatia mapato hayo kutowasilishwa, CAG amewashauri Wakurugenzi wa Mamlaka ya Serikali za Mitaa kuhakikisha fedha zote ambazo hazikuwasilishwa zinawasilishwa na kuwekwa Benki