
Uamuzi huo umetokana na ombi la wanafunzi wawili ambao walikataliwa kujiunga na shule za umma mwaka 2016 na 2010 kwa sababu ya kuwa na rasta
Mahakama katika mji wa kusini wa Zoma imeamuru Wizara kutoa waraka ifikapo Juni 30, ikitangaza kuondolewa kwa vizuizi vinavyowazuia wanafunzi hao kuhudhuria shule za umma
Katika uamuzi wake, mahakama imesema kuwazuia watoto hao kusoma shule za umma ni ukiukaji wa haki ya mtoto ya kupata elimu
Watu wenye imani ya kirasta nchini Malawi kwa muda mrefu wamekuwa wakitengwa na sera za elimu zinazowataka wanafunzi kukata nywele zao ili kukuza usawa miongoni mwa wanafunzi, na kuwalazimu baadhi ya wazazi Warasta kuchagua shule za kibinafsi