
Akizungumza na wanahabari leo Zitto Kabwe amesema kuwa kesi hiyo imetokana na yeye kuzungumzia sakata la IPTL (Kampuni ya kufua umeme) ambapo Seth ameomba kulipwa ‘mabilioni’ ya fedha
"Tuhuma hizo za bwana Seth kwanza si za kweli, kwasababu sijamkashifu na wala kumshushia heshima, lakini ninampongeza sana na kumshukuru kwa ujasiri wake wa kunishitaki kwasababu kesi hii itatoa fursa ya kumaliza jambo hili linaloweka wingu kwa muda mrefu sana katika taifa letu"
"Kesi hii itanipa nafasi ya kuweka ukweli wote wazi na mwisho kuufukia kabisa huu mzoga unaoitwa sakata la IPTL" amesema Zitto akizungumza na wanahabari