
Kamanda wa polisi wa eneo la Nairobi George Sedah amesema wengine wanne walijeruhiwa vibaya kufuatia moto huo
Kamanda Sedah amesema kuwa timu ya pamoja kutoka kikosi cha zima moto cha kaunti na wanajeshi walisaidia kuzuia moto huo kusambaa kwa vitengo vya karibu.
Makumi ya familia zimeachwa bila nyumba zao baada ya nyumba kadhaa kuharibiwa na kuwa majivu.
Wakati huo huo miili ya marehemu imepelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha City.