
Maseneta watajadili kwanza kuhusu pendekezo hilo la jeshi la Congo kabla ya kupiga kura ya siri kuamua hatma ya rais Kabila ambaye Kinshasa inasema anawafadhili waasi na kushirikiana wa AFC/M23
Kamati hiyo maalum yenye wanachama 40 inaoongozwa na Christophe Lutundula, ilikuwa imemwalika Joseph Kabila kufika mbele yake pamoja na mwakilishi wa jeshi la FARDC kujieleza
Licha ya kutakiwa kufika mbele ya kamati hiyo, Kabila alikosa kuheshimu mwaliko wao, Jeshi la Congo linasema rais huyo wa zamani amevunja kifungu cha 136 na 137 ibara ya 3 cha katiba ya nchi kwa kushiriki uasi dhidi ya Jamhuri ya Congo.