
Taarifa ya chama hicho iliyotolewa na kusainiwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi , Brenda Rupia imeeleza kuwa wamechukua uamuzi huo kuwa kwa heshima ya maadhimisho ya Sikukuu ya Eid Al-Adha
"Uamuzi huu ni sehemu ya msimamo wa chama wa kuthamini na kuheshimu mila, tamaduni na imani za wananchi wote, ikiwa ni pamoja na haki ya kuabudu na kusherehekea siku muhimu za kidini katika amani na utulivu" imeeleza taarifa hiyo
Chama hicho kimesema kitaendelea na Operesheni hiyo kesho tarehe 8 Juni 2025, jijini Dodoma kama ilivyopangwa.
"Tunawatakia waumini wote wa Kiislamu Eid Al-Adha njema, yenye amani, mshikamano na baraka tele" imesema taarifa ya chama hicho #EastAfricaTV