Jumanne , 7th Oct , 2025

Wizara ya Kilimo na Umwagiliaji ya Sudan hapo awali iliyata jana majimbo sita yaliyokuwa katika hatari kubwa ya mafuriko ya Nile mwaka huu, ikiwa ni pamoja na Jimbo la Gezira na Khartoum.

Mafuriko makubwa katika Jimbo la Nile nchini Sudan yamesababisha vifo vya zaidi ya watu 30 na maelfu ya wengine kukwama.

Mamlaka zimesema mafuriko ya mito ya Blue na White Nile yameharibu mamia ya nyumba na kuzidisha hali mbaya ya kibinadamu nchini humo. Aidha, zimetoa wito kwa wananchi wanaoishi katika maeneo hatarishi kuchukua tahadhari zote muhimu.

Ukosefu wa vifaa na rasilimali umekatisha mipango ya kupunguza uharibifu huo, huku mvua kubwa ikiendelea kuzuia harakati na uokoaji katika baadhi ya maeneo ya mabondeni. Majimbo mengine yaliyokumbwa na mafuriko ni pamoja na Blue Nile, Al Jazirah na Khartoum.

Wizara ya Kilimo na Umwagiliaji ya Sudan hapo awali iliyata jana majimbo sita yaliyokuwa katika hatari kubwa ya mafuriko ya Nile mwaka huu, ikiwa ni pamoja na Jimbo la Gezira na Khartoum.

Misri kwa upande wake, ambayo pia imeshuhudia mafuriko katika Delta ya Nile, imeinyooshea kidole Ethiopia. Cairo inasema bwawa lake jipya lililofunguliwa kwenye Mto Blue Nile, karibu na mpaka na Sudan, linawajibika kwa kupanda kwa viwango vya maji. Addis Ababa imekanusha kutoa maji ya ziada na kusema bwawa hilo limesaidia kupunguza mafuriko katika eneo hilo.