Katika taarifa ya pamoja ambayo pia ilijumuisha mkuu wa Mkutano wa Wazee wa Afrika Magharibi, maafisa hao walisema nchi ilikuwa tayari kwa tangazo la matokeo ya uchaguzi baada ya kile kilichoelezwa kama mchakato wa taratibu na amani
Waangalizi wa kikanda pia wamekosoa kukamatwa kwa maafisa kadhaa wa ngazi ya juu nchini humo ikiwa ni pamoja na maafisa wa uchaguzi, wakidai waachiliwe huru mara moja.
Wamelezea mapinduzi ya kijeshi ya Jumatano kama jaribio la wazi la kuvuruga maendeleo ya demokrasia ya nchi
Wakati huo huo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ambaye anafuatilia kwa karibu hali hiyo, amewahimiza wale wanaohusika katika hali ya nchini Guinea-Bissau kuonyesha kujizuia na kuheshimu utawala wa sheria



