Jumatano , 3rd Dec , 2025

Msanii Wa Rap Fida Aman ameshare Furaha yake ya kuchaguliwa kuwa balozi wa kusimamia urejeshwaji wa mifumo ya ikolojia na mambo ya mazingira kwa ujumla.Fifi anakuwa balozi wa kwanza Duniani kuchaguliwa katika nafasi hiyo jambo ambalo linaendelea kuiweka sawa Ramini ya Tanzania huko Duniani

Fifi anakuwa balozi wa kwanza Duniani kuchaguliwa katika nafasi hiyo jambo ambalo linaendelea kuiweka sawa Ramini ya Tanzania huko Duniani, Katika Balozi hii Fifi anaungana na mabalozi wengine kama Jason Momoa na wengine wengi ambao wapo chini ya balozi tofauti kupitia UNEP

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Fifi ameandika.........''Ninayo furaha kubwa kupata heshima hii, na ninakubali rasmi uteuzi huu kama Balozi wa kwanza wa UNEP  katika kusimamia Urejeshwaji wa Mifumo ya Ikolojia. Heshima hii ni kubwa kuliko ninavyoweza kueleza. Mazingira yamekuwa msingi wa ustawi wetu na kuyaona yakidhoofika kumezidi kuniaminisha kuwa kila mmoja wetu, mimi nikiwemo, tuna jukumu la kurejesha tunachopoteza.

Ninaishukuru UNEP kwa kuniamini na kunipa nafasi hii muhimu, na kwa kutambua nguvu ya sanaa, utamaduni na vijana katika kuleta mabadiliko ya kimazingira.

Kupitia nafasi hii, najitoa kutumia sauti yangu, jukwaa langu na ubunifu wangu kuelimisha jamii, kuhamasisha utunzaji wa mazingira, na kuhamasisha hatua ndani ya Afrika na zaidi. Nitaendelea kuwaunga mkono wanawake, kuinua vijana na kuhamasisha utunzaji wa mazingira katika kila kazi ninayofanya kuanzia muziki hadi miradi ya jamii.

Huu si tu utambulisho; ni mwito wa kutumikia. Pamoja, tutarejesha mifumo ya ikolojia, kulinda mustakabali wetu, na kujenga kizazi kinachoelewa kuwa kuirudisha asili katika uhai si hiari ni wajibu. Asante sana kwa heshima hii kubwa.''