Jumatatu , 12th Jan , 2026

Shirikisho la soka la Algeria (FAF), limewasilisha malalamiko rasmi kwa Shirikisho la soka Afrika (CAF) na FIFA kuhusu maamuzi yenye utata ya waamuzi baada ya Algeria kupoteza mchezo wake wa robo fainali ya AFCON 2025 dhidi ya Nigeria.

Mwamuzi Issa Sy

FAF limetoa wito kwa CAF kumpiga marufuku mwamuzi wa Senegal Issa Sy na kumuondoa kwenye michuano hiyo mara moja.

Algeria ilipoteza 2-0, kwa mabao ya Victor Osimhen na Akor Adams, na hivyo kuhitimisha kampeni ya mbweha wa Jangwani. Mechi hiyo ilimalizika kwa fujo na mabishano yaliyohusisha Wachezaji na viongozi, pamoja na jaribio la kuvamia uwanjani.

CAF inasema imefungua uchunguzi na kupeleka kesi hiyo kwenye bodi yake ya Nidhamu.