TPA yapokea magari 4397 kwa pamoja
Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) imevunja rekodi kwa kupokea meli yenye magari 4397 ambayo yametoka nchini Japan na hivyo kuwa meli ambayo imepokelewa bandari ya Dar es salaam ikiwa na magari mengi zaidi. Awali, bandari ya Dar es salaam ilipokea meli yenye magari 4041 mwezi April 2022.