Wagundua rubani hakumaliza masomo wakiwa angani
Siku ya jumatatu wiki hii, ndege ya Virgin Atlantic iliyokuwa inatoka mji wa London, Uingereza kuelekea New York, Marekani ilighairisha safari yake na kurudi mji wa London baada ya kugundua moja wa marubani katika ndege hiyo alikuwa hajamaliza mtihani wake wa mwisho wa kuruka na ndege.