Tunaboresha sera za uwekezaji - Dkt. Nchemba
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, amewahakikishia wawekezaji kutoka Uingereza na Norway kwamba Serikali itatoa ushirikiano mkubwa ili kufanikisha uwekezaji wao hapa nchini kwa kuweka mazingira bora ya uwekezaji pamoja na vivutio kadhaa.